Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:18

Zoezi la kuhesabu kura laanza Ghana.


Watu wakiwa kwenye mstari wakisubiri kupiga kura.
Watu wakiwa kwenye mstari wakisubiri kupiga kura.
Wafuatiliaji wa kimataifa wanaripoti kuwa uchaguzi mkuu wa Ghana ulikuwa wazi na wa amani licha ya kwamba upigaji kura unaendelea katika siku ya pili kwa sababu ya matatizo ya kimsingi na kiufundi.

Vituo vyote vya kupigia kura vilifungwa Jumamosi jioni na zoezi la kuhesabu kura lilianza huku kukiwa na zaidi ya asilimia 50 ya kura katika majimbo zilizohesabiwa. Mpaka sasa wapinzani wawili wakuu rais John Dramani Mahama na kiongozi wa upinzani Nana – Akufo –Addo wako sambamba kama kura zinavyokadiriwa.

Ujumbe wa wafuatiliaji ulioko nchini humo unasema zoezi la upigaji kura lilifanyika vizuri. Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo anayeongoza ujumbe huo kutoka jumuiya ya nchi za magharibi ECOWAS anasema mashine mpya za kuhakikisha kura iliharibika na vifaa viliwasili kwa kuchelewa katika vituo vya kupigia kura. Lakini anasema ujumbe wa watu 250 haukugundua chochote kinachoweza kuharibu matokeo.

Bwana obasanjo anasema kuharibika kwa mashine ya kuhakikisha upigaji kura kulitokea kwa sababu betri ilitakiwa kuchajiwa zaidi. Karibu asilimia mbili ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa tena jumamosi ili watu ambao hawakuweza kupiga kura zao ijumaa waweze kupiga kura.

Kiongozi msaidi wa ujumbe huo Dr. Christina Tharpe alisema ECOWAS imetoa wito kwa wagombea kufuata sheria mara kamati ya uchaguzi itakapotoa matokeo .
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa siyo zaidi ya jumanne jioni.
XS
SM
MD
LG