Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:52

FAO yataka serikali kuunga mkono masoko ya chakula duniani.


Mkurugenzi wa shirika la chakula duniani (FAO) Jose Graziano da Silva wakati wa kikao kwenye makao makuu ya FAO Italy.
Mkurugenzi wa shirika la chakula duniani (FAO) Jose Graziano da Silva wakati wa kikao kwenye makao makuu ya FAO Italy.
Idara ya Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linazitaka serikali kuunga mkono masoko ya kilimo ili kukabiliana na ongezeko la bei ya chakula duniani.

Akizungumza Jumanne mjini Roma katika maadhimisho ya siku ya chakula duniani mkurugenzi mkuu wa idara hiyo Jose Graziano da Silva amesema, ni muhimu kuimarisha usimamizi wa chakula kwa sababu hakuna nchi pekee inayoweza kujitosheleza katika dunia ya leo ya utandawazi.

Aliwaambia mawaziri kutoka nchi 20 waliohudhuria kikao hicho kuwa ipo haja ya kuibuka kwa mtizamo mpya wa dunia unaoratibiwa kimataifa kwa kupashana habari na kuwa na uwazi katika masoko, ili kukimu mahitaji ya dunia ya chakula.

Aidha shirika hilo limesema mashirika ya kilimo ya kijamii ni muhimu kwa sababu yana malengo ya kuimarisha jamii zake kwa kutumia raslimali ilizonazo kwa maslahi ya kijamii. FAO linakisia kuwa watu milioni 870 hukabiliwa na njaa duniani, idadi inayosema ni ya juu mno, ingawa imeshuka kutoka watu bilioni moja mapema miaka ya tisini.
XS
SM
MD
LG