Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:28

Tanzania: Chadema kuchukua hatua dhidi ya Serikali


wafuasi wa chadema wakiandamana
wafuasi wa chadema wakiandamana
Nchini Tanzania siku moja baada ya polisi kuzuia maandamnao ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chedema mjini Morogoro na kushutumiwa kuua mtu mmoja kwa kumfyatulia risasi, serikali imesema inachunguza tuhuma kwamba Jeshi la polisi linahusika na mauaji ya mtu huyo

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jumanne kwamba kuna utata wa namna kifo hicho cha mtu huyo anayesadikiwa kupigwa risasi na polisi kwa kuwa polisi mkoani Morogoro imesema ilipata taarifa za kuwepo mtu mmoja aliyejeruhiwa kichwani mita 300 kutoka eneo la tukio.

Waziri Nchimbi ametoa sababu ya polisi kuzuia maandamano hayo ya Chadema na kusababisha kupambana na wafuasi waliolazimisha kuandamana kabla ya kufanyika mkutano wa hadhara wa chama hicho mjini Morogoro..

Bwana Nchimbi alitoa wito kwa vyama vya siasa nchini humo kufuata sheria na taratibu za nchi wakati wa kufanya shughuli zao za kisiasa.

Wakati huo huo katibu mkuu wa Chadema Dk. Willbroad Slaa katika mkutano wake na waandishi wa habari amelishutumu jeshi la polisi kuwa linahusika katika mauaji ya kijana aliyekufa wakati wa maandamano ya chama hicho aitwae Ally Zona kwa kuwa lilitumia hatua zisizofaa za kulazimisha kuzuia maandamano hayo ya amani kinyume cha sheria na taratibu za nchi.

Dk. Slaa amesema Chadema inasubiri taarifa ya daktari anayefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu ili kuweza kuchukua hatua za kisheria.

Alipotakiwa kuzungumzia suala la kuhusika au kutohusika kwa jeshi la polisi katika mauaji ya kijana huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile amesema jeshi lake litatoa tamko rasmi jumatano hii
kutokana na kuchelewa kukamilika kwa uchunguzi wa kitaalamu wa madakatari kuhusiana na kifo hicho.
XS
SM
MD
LG