Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:13

Mali yanuia kuchukua tena udhibiti wa kaskazini


Watu wakiandamana katika mji wa Bamako kupinga makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali kuchukua udhibiti wa kaskazini.
Watu wakiandamana katika mji wa Bamako kupinga makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali kuchukua udhibiti wa kaskazini.
Afisa wa Mali amesema Serikali ya mseto ya nchi hiyo italenga kuchukua udhibiti wa eneo la kaskazini kutoka kwa makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali.

Hamadoune Toure waziri wa mawasiliano wa Mali na msemaji wa serikali ameiambia Sauti ya Amerika kwamba makundi yenye msimamo mkali yanayotaka kusimika sheria kali ya Sharia upande wa kaskazini hawakaribishwi katika serikali mpya ya mseto.

Amesema serikali itaendelea na mipango ya kutafuta msaada ya kulikomboa eneo linalodhibitiwa na makundi ya kiislamu ya Ansar Dine na Mujao ambayo yote yana ushirika na al- Qaida.

Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi - ECOWAS ina mpango wa kutuma wanajeshi wake 3,000 kaskazini mwa mali lakini imesema inahitaji maombi rasmi kutoka serikalini.

Serikali mpya ilitangaza Jumatatu kwamba ina nafasi 31 za mawaziri na kuziba nafasi ya serikali ya mpito iliyoundwa Aprili kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
XS
SM
MD
LG